Hamas ilisema siku ya Jumatatu kuwa Israel haijarejesha usambazaji wa maji kwa Ukanda wa Gaza licha ya kuahidi kufanya hivyo, huku afisa wa Israel akijibu kuwa baadhi ya maji yanatolewa katika eneo la kusini mwa eneo hilo.
Israel iliacha kusambaza maji kwa wananchi wa Gaza kama sehemu ya mzingiro uliowekwa baada ya wapiganaji wa Hamas kuvamia miji na vijiji vyake vya kusini mnamo Oktoba 7. Siku ya Jumapili, Israel ilisema kuwa kama sehemu ya makubaliano na Washington ilikuwa inarejesha vifaa vingine.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Hamas Eyad Al-Bozom alisema siku ya Jumatatu hakujawa na usambazaji wa maji tena: “Wakazi wanakunywa maji yasiyo na afya, na kusababisha shida kubwa ya kiafya inatishia maisha ya raia.”
Msaidizi wa Waziri wa Nishati na Miundombinu wa Israel Israel Katz alisema maji yalikuwa yanatolewa katika jumuiya ya Bnei Sahila, karibu na kusini mwa Khan Younis. Msaidizi huyo alikataa kufafanua kiasi cha maji yanayotolewa.
Katz alisema siku ya Jumapili kwamba kusambaza maji tena kusini mwa Gaza kutawahimiza raia wa Palestina kukusanyika huko wakati Israel inapozipuuza malengo ya Hamas katika mji wa Gaza kuelekea kaskazini.
Israel imewaambia wakazi wa nusu ya kaskazini ya Gaza, ukiwemo mji wa Gaza, kuondoka kuelekea kusini.