Jeshi la Ulinzi la Israel limesema kuwa limesambaza lita 300 za mafuta kwa hospitali ya Al-Shifa, mojawapo ya hospitali kubwa zaidi za Gaza, baada ya kuratibu na wafanyakazi wake lakini Hamas imewazuia kuyakubali.
“Katika saa 24 zilizopita, IDF ilipeleka lita 300 za mafuta kwenye mlango wa Hospitali ya Shifa, lakini mafuta bado hayajaguswa baada ya Hamas kutishia wafanyakazi wa hospitali,” lilisema jeshi la Israel.
Hata hivyo, kundi la wanamgambo wa Palestina lilikanusha kuwa lilikataa mafuta hayo na kusema hospitali hiyo ilikuwa chini ya mamlaka ya wizara ya afya ya Gaza inayosimamiwa na Hamas.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Al-Shifa Muhammad Abu Salmiya alikataa taarifa hiyo ya Israel, kama ilivyo kwa Al Jazeera na kuiita “propaganda”.
“Israel inataka kuonyesha ulimwengu kuwa haiui watoto. Inataka kupaka chokaa sura yake kwa lita 300 za mafuta, ambayo hudumu kwa dakika 30,” Abu Salmiya aliiambia Al Jazeera.