Hamas imeishutumu Israel kwa kukataa ofa zote za kuwaachilia mateka zaidi.
Ilisema Israel ilibeba jukumu la “kuanzisha tena vita na uchokozi”.
Hii inakinzana na taarifa iliyotolewa na Benjamin Netanyahu hapo awali, ambayo ilisema Hamas haikukubali kuwaachilia mateka zaidi.
Hamas iliatangaza kwamba Israel ilikataa pendekezo lake la kuwaachilia wanawake saba na watoto pamoja na miili ya Waisraeli wengine watatu kwa ajili ya kurefusha muda wa kusitisha mapigano ulioanza Ijumaa na kufanyika kwa siku sita kufikia Jumatano.
Israel ilisema itakuwa tayari kuongeza muda wa kusitisha mapigano kwa siku ya nyongeza kwa kila wanawake na watoto 10 wa Israel waliotekwa nyara ambao Hamas inawaachia.
Israel hapo awali ilikanusha madai ya Hamas kwamba haikuweza kuwapata mateka wote huko Gaza, na Palestina Islamic Jihad ilidai uongo kwamba mmoja wa mateka wake aliuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel wakati alikuwa hai na kuachiliwa siku za hivi karibuni.
Wakati huo huo, tawi la kijeshi la Hamas limetoa taarifa na kusema kuwa limeviamuru vikosi vyake kuwa katika hali ya tahadhari kwa kutarajia kufufuliwa kwa mapigano ya kundi hilo la kigaidi na Israel.