Dakika chache kabla ya usitishaji mapigano kukamilika, Hamas imekubali kuongeza muda – muda mfupi baada ya taarifa kama hiyo kutoka Israel.
Qatar, ambayo imekuwa ikifanya kazi kama mpatanishi, ilisema pande zote mbili zimekubaliana siku nyingine ya makubaliano ya muda.
Mazungumzo ya kurefusha kwa mara ya pili yalifikia mapana, na kutoelewana kwa dakika za mwisho juu ya mateka kuachiliwa na Hamas.
Makubaliano hayo ya muda yalikuwa yakirefushwa chini ya masharti sawa na yale ya nyongeza ya kwanza, kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Qatar.
Makubaliano hayo yalihusisha Hamas kuwaachilia huru mateka 10 wa Israel kwa siku badala ya wafungwa 30 wa Kipalestina, na Israel kuruhusu msaada zaidi Gaza.
Kuongezwa kwa muda huo kutawaruhusu wapatanishi kuendelea kufanyia kazi mikataba ya kubadilishana mateka kwa wafungwa.