Hamas inashikilia matakwa yake ya kutaka mazungumzo ya kusitisha mapigano ya Gaza yazingatie makubaliano ambayo tayari yamejadiliwa na Israel na wapatanishi badala ya kuanza upya, afisa mmoja alisema Jumanne, baada ya mashambulizi ya anga ya Israel kuwaua Wapalestina 19 katika eneo hilo.
Marekani ilisema Jumatatu kwamba inatarajia mazungumzo ya amani yaliyopangwa Alhamisi kuendelea kama ilivyopangwa, na kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano bado yanawezekana.
Axios iliripoti kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipanga kuanza safari siku ya Jumanne kwa ajili ya majadiliano nchini Qatar, Misri na Israel.
Serikali ya Israel ilisema itatuma ujumbe kwa mazungumzo ya Alhamisi, lakini Hamas, kundi la wanamgambo wa Kipalestina lililoendesha Gaza kabla ya vita, liliomba mpango unaotekelezeka wa kutekeleza pendekezo ambalo tayari limekubali badala ya mazungumzo zaidi.
Afisa wa Hamas aliambia Reuters kwamba ripoti ya CNN ikisema kuwa kundi lililopanga kuhudhuria siku ya Alhamisi haikuwa sahihi.
“Kauli yetu ya juzi ilikuwa wazi: kinachohitajika ni utekelezaji, sio mazungumzo zaidi,” alisema ofisa huyo ambaye alikataa kutajwa jina lake kutokana na unyeti wa suala hilo.