Hamas imetoa wito kwa Waislamu na Waarabu kote duniani “kuzidisha vuguvugu la halaiki” la kutaka kusitishwa kwa mashambulizi ya Israel huko Gaza, na kufungua kabisa kivuko cha Rafah na Misri ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuvuka.
Kundi hilo lilisema katika taarifa yake linataka wafuasi “kushiriki kikamilifu na kwa bidii katika Ijumaa na Jumapili ijayo”, kwa kutumia kauli mbiu “Fungua kivuko cha Rafah” na “Komesha vita vya maangamizi huko Gaza”.
Mikutano ya wafuasi wa Palestina tayari imefanyika kote ulimwenguni.
Israel inasema inalenga shabaha za magaidi huko Gaza na kwamba haidhibiti kivuko cha Rafah.