Jana September 16, 2016 Mahakama ya Rufani Tanzania, ilitoa hukumu ya kunyongwa mpaka kufa kwa aliyewahi kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mrakibu Msaidizi (ASP) wa Polisi Christopher Bageni, ikiwa ni hukumu ya kosa la matumizi mabaya ya madaraka kulikopelekea vifo vya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva Tax mmoja kwenye msitu wa Pande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Hukumu hii imetolewa baada ya miaka kumi tangu tukio lilipotokea na kusababisha maafisa kadhaa wa jeshi la Polisi kuingia kwenye kashfa ya mauaji hayo, Maafisa hao ni pamoja na aliyewahi kuwa mkuu wa upelelezi wakati huo mkoa wa Dar es salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na wenzake wawili.
Kupitia kituo cha TV cha Azam TV, wakili wa kujitegemea Gabriel Kambona ameutoa ufafanuzi kuhusu hukumu ya kunyongwa ………….
>>Adhabu hii imekuwepo tangu kipindi cha ukoloni na tumeirithi kutoka kwa Wajerumani ambao walikuwa wakiitekeleza adhabu hii ya kunyongwa mpaka kufa, wakimaanisha kwamba mtu anayethibitika kuwa ameua kwa kukusudia basi hukumu yake ni hiyo na mahakama haina uamuzi mbadala kwasababu ni sheria iliyowekwa kwa kifungu cha 195 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai:- Wakili Gabriel Kambona.
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV SEPTEMBER 17 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI