Ikiwa ni wiki moja imepita toka uongozi wa klabu ya Simba utangaze kuachana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, muingereza Dylan Kerr, January 18 kocha wa Dar Es Salaam Young Africans muholanzi Hans van der Pluijm amefunguka na kueleza mtazamo wake juu ya hilo, licha ya kuwa alikaa kimya.
Hans anaamini ni kweli Simba inataka kurejesha heshima yake na kuwa katika nafasi nzuri, ila kwa utamaduni na tabia ya kuendelea kufukuza makocha na benchi la ufundi kwa muda mfupi hafikirii kama itasaidia kitu chochote katika harakati ya kurejesha heshima ya timu hiyo.
“Nafahamu Simba ni timu kubwa na inataka irudi kwenye nafasi yake, lakini nafikiri haikuwa sahihi kumuondoa Kerr wakati huu, ilikuwa ni nafasi ya pekee kwa Kerr kuendelea kuisuka Simba kwa maana haikuwa na matokeo mabovu ya kusababisha kumuondoa kocha, Ila kama mtindo huu utaendelea wa kufukuza benchi la ufundi kila baada ya muda mfupi, sidhani kama Simba itakaa sawa hivi karibuni” >>> Hans van der Pluijm
Dylan Kerr aliyefukuzwa kazi na uongozi wa Simba wiki moja iliyopita kwa madai kuwa haijaridhishwa na uwezo na mwenendo wa timu yao, aliiacha Simba nafasi ya tatu wakati anafukuzwa , huku ikiwa na point 27 katika mechi 13, imeshinda nane, sare mechi tatu na kufungwa mechi mbili.
CHANZO CHA HII STORI: salehjembe
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.