Urusi imeongeza kile inachokiita “harakati za LGBT” kwenye orodha ya mashirika yenye itikadi kali na ya kigaidi, vyombo vya habari vya serikali vilisema Ijumaa.
Hatua hiyo iliambatana na uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Urusi mwezi Novemba mwaka jana kwamba wanaharakati wa LGBT wanapaswa kuteuliwa kuwa watu wenye msimamo mkali, hatua ambayo wawakilishi wa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na waliobadili jinsia walisema wanahofia kuwa ingesababisha kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Orodha hiyo inadumishwa na wakala iitwayo Rosfinmonitoring ambayo ina mamlaka ya kufungia akaunti za benki za zaidi ya watu 14,000 na taasisi zilizotajwa kuwa zenye itikadi kali na magaidi.
Wanaanzia Al Qaeda hadi kampuni kubwa ya kiteknolojia ya Marekani Meta na washirika wa marehemu kiongozi wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny.