Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Harmonize ameachia wimbo mpya unaoitwa “ujana” wenye maadhi yanayofanana na wimbo wake ulitolewa katika mtandao wa You Tube aliotunga spesheli kwajili ya mashabiki wa klabu ya Yanga.
Msanii huyo ameutambulisha wimbo huo kama mbadala wa “yanga bingwa, official yanga anthem” uliotambulishwa wiki mbili zilizopita kuelekea siku ya Mwananchi Day iliyofanyika mapema mwezi huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam.
Harmonize amesema kuwa klabu hiyo tayari ni bingwa, akiwataka mashabiki wa Yanga kuusapoti wimbo huo mpya unaozungumzia ujana ili kupeleka ujumbe kwa vijana ambao wapo katika umri wa kufanya maamuzi ya msingi katika maisha.
Awali msanii huyo aliahidi kutoa “remix” ya wimbo huo na Innoss’B kutoka Kongo, ambaye mwanzoni alikana kuhusika katika kuondoa toleo la kwanza la wimbo wa “yanga bingwa” katika mtandao wa You Tube, hakuna taarifa zozote kuhusu ujio wa “remix” hiyo hadi sasa.
Harmonize amekua msanii asiyetabirika, kupigwa chini kwa “yanga bingwa” bado kunaendelea kuzua maswali kuhusu toleo la wimbo huo kuwa la kwanza, na kuibua wasiwasi kuhusu wimbo wa “ujana” uliotolewa kama toleo la pili kuwa toleo la kwanza.