Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amejitokeza kwa mara ya kwanza jukwaani akiwa na mgombea mwenza Tim Walz mjini Philadelphia, Walz, ambaye ni gavana wa Minnesota aliteuliwa jana na Harris kuwa mgombea wake mwenza wa chama cha Democratic katika uchaguzi wa Novemba.
Mara baada ya kupanda jukwaani, gavana huyo alitoa shutuma nzito dhidi ya mpinzani wao wa chama cha Republican Donald Trump, akihoji kujitolea kwake kwa taifa hilo na rekodi yake ya uongozi. Aidha, amemshambulia Trump kwa kudhoofisha uchumi, kudharau sheria na kuchochea machafuko na mgawanyiko.
Walz anajiunga na Harris ambaye sasa ndiye mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, katika mojawapo ya vipindi vigumu zaidi katika siasa za za Marekani na kuweka mazingira ya kuwepo na kampeni kali na zisizotabirika za uchaguzi wa rais.