Harry Maguire amekubali ombi la msamaha kutoka kwa Mbunge wa Ghana ambaye hapo awali alimkejeli.
Mara nyingi Maguire amekuwa akikosolewa vikali kwa uchezaji wake baada ya kuwa beki ghali zaidi duniani alipohamia United msimu wa joto wa 2019.
Ingawa kutokubalika huko kumekuja kutoka kila pembe ya dunia kwenye majukwaa mbalimbali, angeshangaa kusikia jina lake likichafuliwa katika bunge la Ghana mwaka jana.
Mnamo Desemba 2022, Mbunge Isaac Adongo alidai kuwa Makamu wa Rais Dkt Mahamudu Bawumia ndiye ‘Maguire wa kiuchumi’ kutokana na usimamizi mbaya wa bajeti ya Chama Cha New Patriotic cha Bawumia.
Lakini bungeni siku ya Jumanne, Adongo alirudi nyuma kwa kumdharau Maguire na kuomba radhi kwa beki huyo wa kati wa United.
“Unakumbuka kwamba mwaka jana nilifanya haraka sana kuwaita kaka yangu mkubwa, Dkt Mahamudu Bawumia, Harry Maguire Mheshimiwa Spika, sasa naomba msamaha kwa Harry Maguire,” Adongo alisema.
“Leo, Maguire amepiga kona na ni mwanasoka wa mabadiliko. Maguire sasa anaifungia Manchester United mabao. Mheshimiwa Spika, Harry Maguire sasa ni mchezaji muhimu wa Manchester United.”
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alipost kwenye mtandao wake wa X (awali Twitter) kukubali msamaha na kuongeza ‘tutaonana Old Trafford hivi karibuni’.