Harry na Meghan wamejitokeza huko Windsor Castle kusalimu watu wakati wa siku ya pili ya maombolezo ya kitaifa.
Duke na Duchess wa Sussex waliwasili a Mwana Mfalme na Mkewe wa Wales William kwenye geti la Cambridge mapema jana iioni. Inafikiriwa kuwa ni mara ya kwanza kwa wanandoa hao kuonekana hadharani wakiwa pamoja tangu Machi 2020.
Harry a William hawajaonekana hadharani pamoja tangu mazishi ya Duke wa Edinburgh mwaka jana. Duke alipigwa picha akiondoka kwenye Jumba la Balmoral peke yake lumaa asubuhi baada ya kifo cha bibi yake.
Msemaji wa Prince William alisema alimwalika kaka yake na shemeji yake kuungana naye a Catherine kushuhudia heshima na maua yaliyoachwa nje ya makao ya kifalme.
Vizuizi vva usalama viliwekwa kuzunguka eneo hilo huku umati wa watu – huko Windsor wakitoa heshima zao kwa Malkia Elizabeth II – walilipuka kwa shangwe.
Duke na duchess walishikana mikono wakati wanasoma heshima zilizotolewa na waombolezaji. Wanandoa wote wawili, ambao walikuwa wamevalia mavazi meusi, kisha walitumia dakika 40 kuzungumza na umma.