Klabu ya wekundu wa msimbazi Simba March 16 kupitia kwa mkuu wao wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Haji Manara wametangaza maamuzi mapya kuhusu nahodha wao msaidizi Hassan Is-haka waliyekuwa wamemfungia kwa muda usiojulikana.
Simba wametangaza kumpunguzia adhabu Hassan Is-haka na kwa sasa atapata adhabu ya kufungiwa mwezi mmoja, kupokea nusu mshahara na kuvuliwa unahodha msaidizi, maamuzi hayo yamekuja baada ya kocha wa Simba Jackson Mayanja kuomba apunguziwe adhabu mchezaji huyo.
Is-haka alifungiwa kwa muda usiojulikana na Simba baada ya kumtolea kauli mbaya kocha wake Jackson Mayanja. Hata hivyo Simba pia wametangaza kuwa wataishitaki TFF kwa waziri wa habari, michezo, sanaa na utamaduni Nape Nnauye kutokana TFF kuahirisha sana mechi za Yanga na Azam FC, hivyo ni sawa na kupanga matokeo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE