Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Ikulu Chamwino Dodoma amepokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2019/2020 na taarifa ya TAKUKURU ya 2019/2020
Moja ya vilivyozungumzwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Charles Kichere ni hasara iliyopatikana kwenye Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na amenukuliwa akiyasema haya hapa chini.
“Katika ukaguzi wetu wa mwaka 2019/2020 tumegundua Shirika letu la Ndege limetengeneza hasara mwaka huu ya Tsh. Bilioni 60 na kwa miaka mitano pia limekuwa likitengeneza hasara”
“Kuna changamoto ambazo Serikali inabidi iziangalie ili Shirika letu litekeleze majukumu yake vizuri” — amesema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichere mbele ya Rais Samia Suluhu Ikulu Dodoma leo.
ULIPITWA? TAZAMA HAPA RAIS SAMIA SULUHU AKIPOKEA RIPOTI YA CAG NA KUZUNGUMZA.