Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amesema Hati miliki za Ardhi zinazotolewa kwa wamiliki wa ardhi nchini haziruhusiwi kuwekewa ‘’Lamination’’.
Mhandisi Sanga ametoa kauli hiyo tarehe 18 Machi 2024 wilayani Chalinze mkoa wa Pwani wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii kukagua utekelezaji Mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK) katika eneo la Msolwa .
‘’Hati unayopewa mwananchi hautakiwi kuifanyia lamination, kwanza ijulikane zipo hati za zamani zilizowekewa kitabu kama majalada na zile mpya’’ alisema Mhandisi Sanga.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa wizara ya ardhi, mmiliki wa ardhi anaweza kutaka kuuza ardhi ama nyumba yake kwa mtu mwingine ama kutaka kuchukulia mkopo hivyo hati yake inabidi igongwe muhuri na kama ikifanyiwa ‘’lamination’’ itakuwa ngumu kugongwa muhuri.
Kwa mantiki hiyo, Mhandisi Sanga ameweka wazi kuwa, ndiyo maana wizara yake ya ardhi inashauri hati miliki za ardhi zisifanyiwe ‘’lamination’’ ili mmiliki anapotaka kufanya muamala wowote basi hati yake iweze kufanyiwa.
‘’Lakini hata zile hati milki mpya za kieletroniki hali kadhalika, maana hata hizo zina ‘electronic feature’ .mle ndani yaani kuna vitu vinavyofanya iwe hati ya kipekee lakini pia ina bacon, mambo ya kisasa kidogo hiyyo ukifanya ‘’lamination’’ mambo yote hayo huwezi kuyafanya’’ alisema Mhandisi Sanga.