Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, katika hotuba yake kwenye kikao na wanajeshi wa nchi hiyo amesema “Waranti ya kukamatwa kwa Netanyahu kwa uhalifu wa kivita haitoshi, ni lazima hukumu yake ya kifo itolewe.”
Ayatollah Khamenei kwa mara nyingine tena aliahidi katika hotuba hiyi kwamba “utawala wa Kizayuni utaangamizwa.”
“Waranti ya kukamatwa (ICC) haitoshi, hukumu ya kifo ya Netanyahu lazima iamuliwe,” Ayatollah Khamenei alisema wakati wa mkutano na wanachama wa kikosi cha kujitolea cha Basij cha Iran Jumatatu, katika hafla ya Wiki ya Basij.
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu yenye makao yake makuu The Hague (ICC) imetoa hati za kukamatwa kwa Netanyahu na waziri wake wa vita aliyeondolewa madarakani Yoav Gallant kutokana na uhalifu wao wa kivita unaohusiana na mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza.
Sasa, wawili hao wako katika hatari ya kukamatwa ikiwa watakanyaga katika mojawapo ya nchi 124 zilizotia saini Mkataba wa Roma wa kuanzisha ICC.
Akizungumzia uvamizi wa Israel katika Ukanda wa Gaza na Lebanon, Kiongozi Muadhamu alisema mashambulizi ya mabomu ya nyumba sio ushindi bali ni “uhalifu”.
Adui hajashinda vita vyake dhidi ya Gaza na Lebanon, na kamwe hataweza kufanya hivyo, Ayatollah Khamenei alisisitiza.