Fernando Torres amemaliza kipindi kigumu kabisa cha miaka mitatu na nusu kwenye maisha yake ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kukubali kuondoka katika timu hiyo.
Fernando alijiunga na Chelsea mnamo mwaka 2011 January kwa ada ya uhamisho ambayo ilivunja rekodi ya usajili nchini Uingereza – £50m akitokea Liverpool – leo hii imethibitishwa rasmi kwamba mchezaji huyo sasa anajiunga na klabu ya AC Milan ya Italia kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili.
Torres anajiunga na AC Milan kwenda kurithi nafasi ya Mario Balotelli ambaye amejiunga na Liverpool kwa ada ya uhamisho wa £16m.
Torres ameichezea Chelsea mechi 172 na kufanikiwa kuifungia magoli 45 tangu alipotia mguu Stamford Bridge.
Mchezaji huyo anategemewa kwenda Milan kesho tayari kufanyiwa vipiko vya afya.