Mawakili wa Sean Diddy Combs Jumanne walidai kuwa kesi yake ya ulanguzi wa ngono inaweza kufutwa kutokana na “makosa ya mwendesha mashtaka” yaliyofanywa wakati wa uvamizi wa hivi majuzi katika gereza la mogul huyo wa rap.
Wakati wa kufikishwa kwake katika kesi ya dharura ya mahakama mjini New York siku ya Jumanne, wakili wa Diddy Marc Agnifilo aliwalaumu waendesha mashtaka kwa “kutofaulu kabisa kwa kitaasisi” ambayo wanadai huenda iliweka kesi hiyo hatarini.
Mawakili hao waliendelea kudai kuwa “haki za kikatiba” za Diddy zilikiukwa baada ya maajenti wa shirikisho kukamata kurasa 19 za maandishi za rapa huyo wakati wa uvamizi wa mwezi uliopita na kuzisambaza kwa waendesha mashtaka.
sambamba na hayo Zaidi ya watu kumi na mbili wamefungua kesi dhidi ya rapa huyo wakimtuhumu kutumia ushawishi wake katika tasnia ya burudani kwa kujishughulisha na dawa za kulevya, kuwashambulia na kuwabaka.
Orodha ya hivi punde ya mashtaka ni pamoja na madai ya unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa wanaume wawili ambao walikuwa chini ya umri wa miaka 18 wakati huo.
Diddy, ambaye alikamatwa Septemba 17, amezuiliwa akisubiri kesi ya ulanguzi wa ngono na usafirishaji
Rapa huyo amekanusha tuhuma zote na anatarajiwa kusomewa mashtaka mwezi Mei.