Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kawe ambaye kwa sasa ni mbunge Viti Maalum kupitia CHADEMA, Halima Mdee amesema licha ya maneno mengi kuzuka kuwa yeye amenunuliwa, yeye hawezi kununuliwa na mtu wala chama chochote sababu thamani yake ni kubwa kuliko mtu au chama chochote cha siasa.
“Hatukudharau kikao, tuliomba tu Wiki moja mbele, Mbowe amenijenga Mimi, ametujenga, inawezekana kuna Vijana wana ya kwao lakini kuna Viongozi tunawaheshimu sana kwasababu wana mchango mkubwa wa sisi kuwa hapa, lakini hatimaye tumevuliwa Uanachama” Halima Mdee
“Sisi tumefukuzwa ila tutakuwa Wanachama wa hiyari, ndio maana tumevaa gwanda za CHADEMA, mamlaka za rufaa zipo Baraza Kuu, jana jioni tumepata barua ya taarifa ya uamuzi, mchakato wetu wa rufaa tutaanza kuutafakari ili tuangalie namna ya kutatua tatizo” -MDEE
“Tunaipenda CHADEMA, tunaiheshimu CHADEMA, hatutoondoka CHADEMA, tutabaki Wanachama wa hiyari mpaka tutakapomaliza mchakato wa ndani ya Chama wa kumaliza matatizo yetu, naamini tutayajenga ndani kwetu, leo sizungumzi nje na kuongeza matatizo” -MDEE
“Tuna dhamira za kuchukua hatua za Kikatiba ndani ya Chama chetu na hatua nyingine kwa kadri ambavyo tutaona zina afya kwa pande zote mbili, na kwakweli nimetukanwa sana na hili limenisadia kujua Marafiki wa kweli na wale ambao walikuwa wananisikilizia” -MDEE