Mzee Ernesto Kapinga wa Njombe Tanzania alizungumza na sisi siku kadhaa zilizopita na kutuambia sababu za yeye kuamua kuoa Wake 16 na kuishi nao wote ndani ya eneo moja huku akisema idadi kamili ilikua Wake 20 lakini wawili wakafariki na wawili wakamkimbia.
Kama ulipitwa Intervie ya Mzee Ernesto ipo chini ya hii ya Wake zake lakini kwa ufupi tu Mzee huyu alisema aliamua kuoa Wake wengi kutokana kwanza na agizo la Mungu la kuijaza dunia, lakini pia Baba yake Mzazi alimwambia inabidi apate Watoto wengi sababu ukoo wao ni mdogo hivyo anatakiwa afanye kazi ya kuukuza, pia
Pengine ungetamani kusikia kutoka kwa baadhi ya Wake zake wakizungumza kwenye hii habari ambayo sio ya kawaida na wala sio idadi ya Wake tuliyozoea kuiona, Millard Ayo ameongea na baadhi yao akiwemo Mke ambae ni sehemu ya Wake saba kwenye hao 14 ambao wameolewa Mtu na Dada yake, bonyeza play hapa chini kutazama Interview nzima.
EXCLUSIVE: MZEE ERNESTO ANAYEISHI NA WAKE 16 KWENYE ENEO MOJA “WAMENIPENDA WENYEWE”