Moja ya matukio ambayo yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara ni pamoja na kujiua ambapo mara nyingi yanaripotiwa kutokana na kusababishwa na mambo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi lakini mara nyingi ambao huhusishwa na matukio hayo ni watu wazima.
Vifo vya watoto kutokana na kujiua ni jambo lisilo la kawaida katika jamii lakini hata hivyo Marekani imetajwa kuwa kinara kwa watoto kujiua duniani.
Kituo cha kudhibiti magonjwa Marekani kimegundua kuwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 13 hujiua kwa wastani wa kila baada ya siku tano huku wengi wakiwa ni watoto wa kiume.
Unaambiwa kati ya mwaka 1999 hadi 2015 zaidi ya watoto 1, 309 wenye umri wa kati ya miaka 5 hadi 12 walijiua huku sababu kubwa ikitajwa ni sababu za mahusiano ikiwa ni pamoja na kuzozana na rafiki zao, ndugu na wakati mwingine wapenzi wao.
Hali ya Ester Bulaya akiwa Hospital baada ya kuugua akiwa rumande…tazama kwenye video hii hapa chini!!