Kama utakua ni mpenzi wa kutazama taarifa ya habari na hukupata time ya kutazama taarifa ya Habari April 28 2016 kupitia TV za Tanzania usijali millardayo.com imekurekodia habari 9 kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka Clouds TV…Makandarasi wa hovyo waadhibiwe
Wakati mji wa Dodoma ukiwa mkavu na haujapata mvua kwa wiki zaidi ya mbili huku Jiji la Dar es likiwa na idadi kubwa ya mvua Mbunge wa Ukonga amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwachukulia Hatua Makandarasi wote ambao wamechangia maji kupoteza muelekeo……..
>>>’Maeneo ambayo yameathirika zaidi katika Jiji la Dar es salaam ni pamoja na Jimbo la Ukonga barabara ya kutoka Banana, Kitunda na Kivule Msongora hivi sasa ninavyoongea sasa hivi mawasiliano yamekatika kwenye barabara hizo‘;-Mwita Waitara Mbunge wa Jimbo la Ukonga
Habari kutoka Clouds TV…Maji yamesababisha Ulemavu
>>>’Sisi tulikuwa tunachota maji katika bomba ndio wakatokea watu wakatuambia tutoke na tuache kuchota maji eneo hilo ndipo tulipowaambia kuwa ili bomba sio lenu, wakatukimbiza waliponikamata ndio wakanipiga mpaka nimevunjika mguu wangu‘:–Asha
Habari kutoka ITV…Mafuriko
Mvua yakwamisha shughuli na kusababisha kero Jijini Dar es salaam….>>>‘Hii hadha ya maji kuingia mpaka ndani ni kutokana na waliojenga barabara kutokuweka mifereji ya pembeni katika barabara‘:-Mkazi wa Jiji la Dar es salaam
Habari kutoka Star TV… Ajali ya Barabarani Singida
Watu wawili wamefariki na watano wamejeruhiwa kutokana na ajali iliyotokea Mkoani Singida…..
>>>’Ajali imetokea kwenye barabara kuu ya Kutoka Singida kwenda Mwanza katika eneo la njiapanda hapa kwenye T, ajali imetokana na uzembe wa dereva wa bus la Nkondo express‘:-ACP Simion Haule Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida
Habari kutoka Star TV…Jaribio la Uhalifu
Watu watatu wauawa na Polisi Mbeya……
>>> ‘Katika majibizano ya risasi ya majambazi hao na Polisi, Jambazi mmoja aliyekuwa na silaha aina ya SMG alipigwa risasi na kuuawa na Polisi kwa kupigwa na risasi eneo la tumboni na miguuni na jambazi huyo alifahamika kwa jina la Baraka’;-SSP. Butusyo Mambelo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Habari kutoka TBC1…Watendaji wa Vijiji Waagizwa Kuwasaka Wazazi wa Wanafunzi Watoro
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Shabani Kisu amesema kitendo cha wanafunzi kuacha masomo wakati Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kuwalipia ada bure hakikubaliki kabisa …………
>>>’Hawa wazazi ambao watoto wao ni watoro lakini hatimaye wameanza kuja shule sasa, muakilishi wa OCD naomba hawa muachukue muwapeleke kituo cha Polisi kwa ajili ya kutoa maelezo kwanini wameshindwa kuwasimamia watoto wao kwenda shule‘:-Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Shabani Kisu
Habari kutoka TBC1…Idadi ya Watumishi Hewa Yaongezeka
>>>’Nimewapa wakuu wote wa Idara siku saba ifikapo tarehe 4/o5 wawe wameniletea ripoti kwenye meza yangu kuonyesha ni watumishi wangapi ambao wamehamishwa majukumu yao bila kufuata utaratibu na ni hasara kiasi gani Serikali imeingia kutokana na uhamisho huo‘;-Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi
Habari kutoka Azam TWO…Wapinzani Wang’ang’ania Bunge Live
Wabunge wa upinzani leo wameitaka Serikali kuruhusu Bunge kwenda Live huko mjini Dodoma…..
>>>’Ni kitendo cha kushangaza na cha ajabu ambacho Serikali hii toka imeingia madarakani yaani jambo kubwa la ubunifu ambalo wamelifikiria ni kuhakikisha wanazima matangazo ya moja kwa moja ya bunge ili wananchi wasiweze kulitazama Bunge‘;-Mbunge
Habari kutoka Channel 10…Makampuni ya Wachina Nchini
Yawasaidia wafanyakazi bora wa Tanzania
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIIKOSA YA ZITTO KUHUSU UTUMBUAJI MAJIPU NA BUNGE KURUSHWA LIVE? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI…