Habari zote zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya August 16 2016 usijali Millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tano ‘Hot‘ kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka TBC
Jeshi la Polisi lapiga marufuku uvaaji wa sare kwa wananchi wasio wanajeshi kamshina msaidizi wa Polisi Advera Bulimba ameyazungumza haya katika kutoa ufafanuzi juu ya onyo la serikali kwa wananchi
>>>‘Sisi kama serikali tunatoa onyo kwa mtu yeyote au kikundi chochote kitakacho tumia sare ama vazi lolote lile linaloshaabiiana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama kuacha mara moja na atakae bainika kufanya vitendo hivyo hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria kuhakikisha kwamba linakuwa fundisho kwa wengine’
Habari kutoka Azam TV
TRA kuhakiki Tin
TRA kufanya uwakiki wa walipa kodi ili kubaini walipa kodi hewa ambapo kwenye mfumo wa awali wamebaini kulikuwa na mapungufu ikiwa mtu mmoja kumiliki zaidi ya tini moja jambo ambalo wanataka kulibadili.
>>> ‘Tunataka kuboresha huduma ya ulipaji kodi na tuongeze ufanisi katika swala zima la usimamizi, ukusanyaji wa mapato katika kiwango ambacho kinastahiki lakini pia tunataka tuwawezeshe wananchi wetu kupunguza gharama za ulipaji kodi kwasababu mfumo wetu sasa utakuwa ni utawawezesha kutekeleza wajibu wao kwa hiari zaidi’ – kamshina Mkuu TRA (Alphayo Kidata)
Habari kutoka ITV
Hospitali ya Rufaa KCMC Moshi yakabiliwa na tatizo la msongamano wa wagonjwa
Katika kipindi cha mwaka 2015 mpaka 2016 hospitali hiyo imelazimika kutoa msamaha wa zaidi ya shilingi milioni mia tatu ya wagonjwa walioshindwa kulipia gharama za matibabu.
Habari kutoka Azam TV
Ziara ya waisrael taasisi ya moyo
‘Sisi model tuliyoitumia iko tofauti kidogo wanaleta wao madaktari hapa kufundisha kwasababu unaweza kufundisha madaktari wengi zaidi na kufundisha wauguzu wengi zaidi kwa wakati mmoja na kufanya operations nyingi zaidi kuliko kumpeleka mtu kule kuepuka gharama nyingi‘- Mkurugenzi mkuu taasisi ya moyo (Prof. Mohammed Janabi)
Habari kutoka Azam TV
Rais Magufuli afanya ziara na mkewe kuwatembelea na kuwaombea Spika wa Bunge aliyekuwa India kwenye matibabu Ndugai pamoja na aliyekuwa Waziri mstaafu John Malecela, wamemshukuru sana Rais na kutaja kuwa wanaendelea vizuri na matibabu na wamepata huduma nzuri kwa madaktari.
ULIKOSA KUIONA VIDEO YA KINACHOFUATA BAADA YA MAJINA TISA KUPITISHWA KUMRITHI PROF.LIPUMBA CUF? UNAWEZA ITAZAMA VIDEO NIMEKUWEKEA HAPA CHINI