Habari zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya August 17 2016 usijali Millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tano ‘Hot‘ kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka Channel TEN
Aliyekuwa mkurugenzi wa wizara ya vitambulisho vya taifa NIDA Dickson Maimu na wenzake saba wamekabiliwa na mashtaka 27 ikiwemo matumizi mabaya ya ofisi ya madaraka pamoja na kuhujumu uchumi na tayari wamefikishwa mahakama ya kisutu.
Habari kutoka Clouds TV
Kwasasa watanzania wanaotumia mitandao wamekadiriwa kufika zaidi ya million 17 ikiwa ni uongezekai wa watu million 12 kutoka million 5 mwaka 2011.
Kumekuwa na matumizi mabovu yamitandao ya kijamii ikihusisha utapeli mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA wametoa onyo kwa wanao tumia mitandao vibaya watashughulikiwa.
Habari kutoka Channel TEN
Imebainika kuwa na wanafunzi hewa na ubadhilifu pesa za mikopo kwenye vyuo 31 kati ya vyuo 81 hapa nchini vilivyofanyiwa utafiti na kubaini jumla ya shilingi Billion 3.8 imekuwa haifiki kwa wanafunzi husika bali hewa katika mwaka wa fedha 2015 mpaka 2016
>>>’Uchunguzi zaidi utafanyika yani hili swala la bodi ya mikopo hatutalifumbia macho kwasababu yani kila tukifanya uchunguzi unakuta linahitaji ulazima wakuingia ndani zaidi na mi nasema kwamba tutaendelea kuingia ndani zaidi mpaka kieleweke‘ – Prof Joyce Ndalichako
Habari kutoka ITV
Rais Magufuli amekutana na kiongozi wa madhehebu ya Bohora Duniani Ikulu Dar es salaam na kumtaka kiongozi huyo kuihamasisha nchi yao kuwekeza hapa nchini ususani katika viwanda sambambamba na kufanya biashara nchini Tanzania.
>>>’ Napenda nitoe wito kwamiliki hii ya mambo haya mje mfanye biashara Tanzania kwa wingi kwasababu tumepanga kwa ya kipindi cha kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 na 2021 Tanzania iwe nchi ya viwandakwahiyo tunawakaribisha kuja kuanzisha viwanda hapa nchini, nataka kila mahali pawe na viwanda tutakapokuwa na viwanda na uwakika watanzania wengi maskini wataat ajira‘- Rais J.P.Magufuli
Habari kutoka ITV
Operesheni dhidi ya uvuvi haramu
>>>’ Uvuvi haramu Rais alishaelekeza sisi wala hathangaiki kufanya maboresho yoyote wala kijaribu kuongeza na akili zetu, maelekezo yake yalikuwa wazi sis tunayafanyia kazi hivyohivyo yalivyo‘- Mkuu wa mkoa wa Mwanza (John mongela).
ULIKOSA KUIONA VIDEO YA WAKUU 90 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUFUKUZWA WILAYA YA KINONDONI? UNAWEZA KUITAZAMA VIDEO NIMEKUWEKEA HAPA CHINI