Inawezekana umewahi kusikia watu, wanaharakati au hata wataalamu wa afya wakionya suala la wanawake hata wanaume kuchubua ngozi zao ili wawe weupe na kueleza madhara ya kufanya hivyo.
Nchini Nigeria wanawake wamepewa onyo la kutotumia vidongo vya kuchubua ngozi zao kwani huwachubua hadi watoto waliopo tumboni kipindi wanapokuwa wajawazito.
Wataalamu hao wa afya wameeleza kuwa kufutia kuchubua ngozi za watoto hao tumboni pia dawa hizo haramu zinapelekea madhara ya uzazi ikiwemo viungo vya ndani vya mtoto kuharibika.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini humo (FDA) dawa hizo zimekuwa zikiingizwa nchini humo kinyemela kwani mamlaka hiyo hairuhusu aina ya vidonge vya kuchubua ngozi ambavyo pia huchubua ngozi ya mtoto aliye tumboni.
FULL VIDEO: SUGU NA MASONGA WAKIPELEKWA GEREZANI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA