Moja ya habari ambayo imekuwa gumzo ni hii inayotokea Kilimanjaro ambako Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro imemhukumu kifungo cha maisha jela mfanyabiashara wa Madini Benedict Kimario kwa makosa mawili ya ubakaji na ulawiti.
Mtu mmoja amefariki na wengine wanne wa familia moja wamelazwa hospitali baada ya kula muhogo unaodaiwa kuwa na sumu katika kijiji cha Masigati kilichopo Manyoni, Singida.
Hizi hapa zote stori kubwa kutoka kwenye Magazeti ya Tanzania leo July 22, 2017…zipitie.
Mtu mmoja amefariki na wengine 4 wa familia moja wakazi wa Masigati, Singida wamelazwa baada ya kula mhogo unaodaiwa kuwa na sumu. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Serikali imetangaza rasmi kufutwa kwa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), kuanzishwa Tume ya Madini na kuongeza malipo ya mrabaha. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Waziri Mkuu Majaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote kusimamia biashara ya mazao ya kilimo. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kilimanjaro imemhukumu kifungo cha maisha jela Benedict Kimario kwa makosa mawili ya ubakaji na ulawiti. #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Polisi imesema vitendo vya unyang'anyi vimepungua lakini hali ya vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa watoto wadogo ni mbaya. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kumshikilia Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.#UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
"Haku maana kama wasanii wetu waliokuwa nominated kwenye tuzo za nje, kama tuzo hazitawapa faida kibiashara." – Ruge Mutahaba. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
"Nimezaliwa kwa ajili ya Watanzania, kama baya lolote linanitokea linitokee kwa ajili ya Watanzania." – Rais Magufuli. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Huku takwimu za TRA zikionesha wa Tsh tril 1-1.3 makusanyo ya kodi kwa mwezi Rais JPM amesema nguvu ikiongezwa yatafikia tril 2. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Jeshi la Polisi Pwani linawashikilia wahamiaji haramu 44 kutoka Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Polisi Rukwa inamshikilia mwalimu wa Miangalua Sec, Sumbawanga akituhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa Form 3 mwenye miaka 16. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Rais JPM amesema ataifungia migodi kama wawekezaji watachelewa kufanya mazungumzo ya kurejesha fedha walizochukua kwa ufanganyifu #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Wasichana wawili wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Temeke wakikabiliwa na mashtaka ya kufanya biashara ya kuuza miili yao. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa miezi 3 kwa wananchi waliojenga nyumba ndani ya eneo la mpaka wa Tanzania na Zambia kuzibomoa. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Watu 45 wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma mbalimbali akiwemo Harison Mkoka anaetuhumiwa kuwalewesha wanawake kisha kuwabaka. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
TRA imekusanya Tsh. Bilioni 32.5 ya kodi ya majengo kwa mwaka wa fedha 2016/17 kutoka katika Majiji, Miji na Manispaa 30. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Kiwanda cha ngozi Mwanza Tanneries kinachodaiwa kumilikiwa na Yusuf Manji kimefungwa kwa kutoendelezwa kwa zaidi ya miaka 5. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
Serikali imesitisha utoaji wa leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini hadi pale Tume ya Madini itakapoundwa kufanya kazi. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 22, 2017
FULL VIDEO: Fatma Karume Wakili wa Lissu aongea kinachoendelea…tazama kwa kuplay video hii!!!!