Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) leo March 14, 2018 imetoa wito kwa Watanzania wenye taaluma na ujuzi kwenye sekta ya mafuta na gesi kujitokeza na kuchangamkia fursa katika Mradi wa Ujenzi wa Bomba la kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania.
Watanzania wenye sifa wameshauriwa kujitokeza na kujisajili TaESA ili serikali ijue idadi halisi ya watu wenye sifa na walio tayari kuajiriwa katika mradi huu wa ujenzi wa bomba la mafuta. Inaelezwa kuwa zoezi la usajili ni bure.
Zoezi la usajili linafanyika kwa kujaza fomu zinazopatikana katika tovuti ya www.taesa.go.tz au kufika kwenye ofisi za kanda zilizopo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Mwanza.
Mradi huu ambao utachukua miezi 24 hadi 36 kukamilika, unatarajiwa kuzalisha fursa za ajira 10,000 wakati wa ujenzi wa 1,000 wakati wa uendeshwaji wake.
Umoja wa Mataifa kuingia mkataba na Serikali kupitia Maafisa habari