Jiji la Dar es Salaam ndilo linaloongoza kwa kuwa na joto sana kwa Tanzania na kuna kipindi watu hulalamika uwepo wa joto kali na wengine kulazimika kulala nje wakati wa usiku ili kuepukana na adha hiyo.
India iliingia kwenye headlines baada ya kutokea kwa vifo vya watu zaidi ya 500 kutokana na kuongezeka kwa joto lililofikia nyuzijoto 48.
Stori nyingine inayofanana na hiyo imetokea Pakistani ambapo mpaka sasa watu 700 wamefariki kutokana na ongezeko la joto lililofikia nyuzijoto 45 huku Waziri mkuu wa nchi hiyo, Nawaz Sharrif akitaka hatua za dharura zichukuliwe mara moja kukabiliana na hali hiyo.
Tayari Jeshi limepelekwa katika eneo la Kusini mwa mji wa Karach ambako idadi kubwa ya vifo imetokea na kujenga vituo vya kukabiliana na joto hilo ili kuisaidia Mamlaka ya kukabiliana na majanga ya dharura.
Watu walioathirika zaidi ni watu wazima ambao wana kipato cha chini huku wengine wakiwa katika hali mbaya.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.