Hekaheka ya leo Desemba 10 inatoka Vingunguti Dar es Salaam, ambapo jamaa mmoja alitoa posa ya kuoa msichana mmoja lakini baada ya kuonekana akisuasua kuoa wazazi wa msichana huyo waliamua kupokea posa ya mtu mwingine na kuruhusu binti yao aolewe.
Baadhi ya watu wa karibu na familia hiyo wamesema kuwa jamaa huyo amekuwa akiahirisha mara kwa mara suala la kuoa na baadaye akawaambia kwamba ameahirisha hana mpango wa kuoa na akagoma kurudishiwa hela aliyoitoa kwa ajili ya posa.
Siku ya ndoa jamaa huyo alikuja na Polisi na kupelekea mtafaruku mkubwa ambapo baada ya Polisi kusimuliwa kilichotokea waliwaacha waendelee na shughuli hivyo kufanya jamaa huyo akose mke, japo watu wa karibu wamesema jamaa huyo tayari ana mke wa kwanza hivyo hawajajua sababu iliyomfanya aahirishe zoezi lake la kuoa mke wa pili.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook