Hekaheka ya leo December 17 inatoka Ubena Zomozi, Morogoro ambapo mtu mmoja aliumwa na kusafirishwa kuja kutibiwa Muhimbili, baadaye akafariki.
Ndugu walionekana kutoridhishwa na mazingira ya kufariki kwa ndugu yao wakihusisha na imani za kishirikina hivyo wakaamua kumtafuta mtaalamu ambaye aliwaambia angefanya utaratibu ili kumrudisha ndugu yao.
Polisi walitaka kumkamata mganga huyo lakini wanakijiji waliomba aachiwe ili amalize shughuli hiyo.
Baada ya kufanya dawa mganga huyo aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu, japo mashuhuda wanasema mganga huyo tayari alishamtoa mtu huyo lakini aliwapa sharti la kutomfunua hivyo hakuna aliyehakikisha kwamba ni kweli mtu huyo alikuwa amerudishwa ama hapana.
Mwenyekiti wa Kijiji alithibitisha kwamba naye kashuhudia kila kitu ila hakuona kama mtu huyo aliyerudishwa ndiye aliyefariki au sio yeye, ila alivyomuona hakuona kama alikuwa anapumua.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook