Hekaheka inaendelea leo, ilianzia jana ile stori ya mwanamke ambaye alikutwa katika Hospitali ya Mwananyamala ndani ya wodi ya wanawake waliojifungua katika hekaheka za kutaka kuiba mtoto mchanga !!
Muuguzi mmoja kutoka Hospitalini hapo amesimulia jinsi ambayo ilikuwa.. amesema daktari moja alimshtukia baada ya kumkuta akiongea na simu maongezi ambayo yalimpa shaka.. katika kuchunguza ndio wakajua kwamba alikuwa na lengo la kuiba mtoto.
Wanawake wenzake ambao walikuwa wamelazwa kwenye wodi hiyo wamesema kuwa kila wakati alionekana kama anataka wenzake walale ili aibe mtoto, kuna wakati alionekana kumtaka mtoto ambaye alifariki ili awadanganye ndugu zake kwamba mtoto aliyejifungua amefariki.
Wakati wote akiwa ndani ya wodi hiyo alikuwa akiwasiliana na ndugu zake na kuwaambia kajifungua mtoto njiti na ndugu hawaruhusiwi kumuona mtoto kwa sasa.
Baada ya kumshtukia taarifa ilipelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay ambako mwanamke huyo anashikiliwa mpaka sasa.
Leo amesikika Muuguzi kutoka Hospitali ya Mwananyamala, kesho atasikika mama mkwe na mume wa mwanamke huyo.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.