Kwenye Leo Tena ya CLOUDS FM leo alikuwepo staa wa comedy Bongo, anaitwa Kingwendu.. story zilikuwa nyingi ikafikia kwenye Hekaheka akatoa hii ambayo kwa upande mwingine ni kwamba hata yeye anaonekana kujutia, ilibaki kidogo apoteze uhai wake yeye mwenyewe!
Kingwendu alipata mkasa huo wakati anasoma shule ya msingi, siku moja alikuwa na njaa sana akaenda kuiba machungwa kwenye shamba la shule, mwalimu wake akamuona akapiga kelele kwamba kuna mwizi shambani, kundi la wanafunzi wakaanza kumkimbiza.
Kwa bahati mbaya alianguka na kujichoma kisu mkononi, ilikuwa ni kama bahati tu kupona kwa kuwa kingemchoma tumboni huenda hali ingekuwa tofauti.
Kisu hicho alikuwa amekibeba kwa ajili ya kuonjea machungwa akiwa juu ya mti, baada ya kumkuta hilo anasema akaacha kabisa udokozi.
Kusikiliza story yote bonyeza play hapa mtu wangu…
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook