Kulikuwa na stori ambayo iliwahi kusikika kwenye Hekaheka kutoka Mabibo Dar, msichana mmoja alifanyiwa ukatili wa na kuuawa na watu wasiofahamika, mwili wake ukatupwa kichakani maeneo ya Mabibo.
Mama wa mtoto huyo amesema binti yake hakuwa na tabia ya uzururaji, mara nyingi alikuwa anakaa ndani ya nyumba yao baada ya kutoka shule.
Siku ya tukio msichana huyo alikuwa nyumbani kwao akijisomea, akatoka muda wa saa 12 jioni, mama huyo akajua mtoto wake hajaenda mbali lakini muda ulipozidi kwenda na msichana huyo hajarudi walipata wasiwasi na kuanza kumtafuta.
Siku ya pili walipata taarifa za maiti iliyokutwa imetupwa, walipoenda Hospitali ya Muhimbili walikuta mwili wa mtoto huyo ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali.
Mama mdogo wa msichana aliyeuawa alisema alikutana na msichana huyo akiwa ameongozana na kijana mmoja lakini hakuwa na wasiwasi wowote, alipochelewa kurudi wakaanza kumtafuta bila mafanikio na kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi Buguruni, siku ya pili yake wakaletewa taarifa za mwili wake kukutwa umetupwa.
Kusikiliza Hekaheka yote bonyeza play hapa chini…
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook