Hekaheka hii imeendelea kwenye ile ambayo ilisikika jana JUNE 03 2015.. Ishu ilikuwa mwanamke mmoja kukamatwa akiwa na jitihada za kutaka kuiba mtoto mchanga katika Hospitali ya Mwananyamala Dar.. kisa akasema kwamba ndugu wa mume wake wamekuwa wakimlazimisha azae.
Mama mkwe wa mwanamke huyo ameongea leo, amesimulia ilivyokuwa kwamba waliwahi kumpeleka Hospitali lakini akawatoroka.. baada ya siku mbili akawapigia simu kwamba yuko Hospitali ya Mwananyamala amejifungua mtoto njiti.. mama mkwe akapata hofu kwa vile hakuwa anaonekana kama ni mjamzito.
Baadae katika kufanya mawasiliano wakampata daktari wa Hospitali hiyo na kumwomba awe makini na mwanamke huyo kwa vile wanahisi hana lengo zuri.. baada ya kufika na kumhoji alikubali kwamba ni kweli alikuwa kwenye mpango wa kuiba mtoto.
Bado mwanamke anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.. sehemu nyingine ya Hekaheka hiyo ni kesho, Geah Habib kasema kesho atasikika mume wa mwanamke huyo.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.