Kwenye stori ya Hekaheka leo ni ya JB kuhusu utapeli, amesema wakati akiwa nyumbani hana kazi baada ya kumaliza masomo, alipewa jukumu la kuangalia kuku na kuuza, siku moja akaja mteja anataka kuku , mteja mwenyewe alikuwa tayari kuchukua kuku wote 600.
Kabla ya dakika 5 kuisha ikaja gari kupakia kuku, anasema kuku wote wakawekwa kwenye gari, wakati anaomba hela yake baada ya kumaliza kupakia akaambiwa atapewa baada ya kufikisha kuku wote sehemu husika maeneo ya Temeke.
Ishu ikaendelea wakaongozana mpaka Temeke, wakafika sehemu ambapo jamaa alishuka pamoja na kuku wote wakashushwa…. JB akaambiwa amsubiri mteja wake nje ili amletee hela… muda mrefu ukapita mteja hata hatokei, kuingia ndani alikuta jamaa hayupo na mtu aliyemwagiza kufata kuku jamaa huyo alimalizana nae tayari, yani alishapewa hela ya kumlipa JB lakini akatokomea nayo na kumuacha JB mikono mitupu !!
Msikilize hapa akizungumza kwenye Hekaheka…
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos