Jana kulikuwa na Hekaheka kutoka Kurasini Dar iliyokuwa inahusu ishu ya mzee moja kudaiwa kuwajeruhi kwa risasi watu wawili, baadae wakavamia watu ambao walifanya vurugu na kuchoma moto gari la mzee huyo alafu wakawa wanataka kuchoma moto na nyumba ya mzee huyo pia.
Mashuhuda waliongea jana, tuhuma na lawama zao walizipeleka kwa mzee huyo kwamba ni kawaida yake kuwatishia bastola watu wanaopita jirani na nyumba yake au wanaompigia kelele.
Leo kasikika mtoto wa mzee huyo ambae amesimulia hali ilivyokuwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho.. mtoto huyo amesema kuwa baada ya baba yake kuokolewa na Polisi watu hao walivamia tena nyumba hiyo wakamjeruhi mtu mmoja ambae aliachwa na Polisi kwa ajili ya kulinda.. wao walikuwa kwenye uvungu wa kitanda pamoja na ndugu zake wengine wakati ishu yote inatokea.
Mtoto huyo amesema nao pia walivamiwa na kundi la watu, wakawa wanatishia kuwanyang’anya simu na hela, baadae nao wakaja kuwaokoa, wakatoa na vitu vingine vyote kwenye nyumba.
Hapa iko sauti ya Hekaheka ya leo mtu wangu, play umsikie mtoto huyo akisimulia ilivyokuwa.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.