Kama ilivyo kawaida ya Hehaheka imekuwa ikituweka karibu na matukio ambayo yanatokea kwenye maisha ya watu ya kila siku, leo inahusu tukio la mama na mtoto wake kukutwa ndani wakiwa wamefariki maeneo ya Mburahati, Dar es Salaam.
Baba amesimulia na kusema tukio hilo limemsikitisha sana kwa kuwa hakutegemea kumpoteza mke wake na mtoto wao kwa wakati mmoja lakini anaamini ni mipango ya Mungu.
Baba huyo amesimulia kwamba siku moja asubuhi mke wake alianza kulalamika anaumwa tumbo na alianza kuharisha, yeye ikabidi aende Duka la Dawa kumnunulia dawa… wakati huohuo mtoto wao pia alikuwa anaharisha, wote wawili wakatumia dawa za Malaria.
Baada ya muda kidogo mama na mtoto wake walifariki, Hospitali manesi wamesema kwamba wagonjwa wote wawili walikuwa na Ugonjwa wa Kipindupindu.
Stori yote kwenye Hekaheka nimeirekodi na kukuwekea hapa, Baba aliyepatwa msiba amesimulia kila kitu.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE