Hekaheka ya leo inatokea maeneo ya Mbagala ambapo kuna mama mmoja anatuhumiwa kumnyonyesha mtoto wa jirani yake…alimchukua mtoto wa jirani yake huyo na kumnyoshesha baada ya kumkuta analia.
Dada wa kazi kazungumza na Geah Habib na kusema alikua anapika akaona jirani yake amekuja na kumchukua mtoto na kuanza kumnyonyesha baada ya kumuona analia.
Mama mzazi wa mtoto amezungumza na kusema alirudi kutoka kazini na kupewa taarifa hizo..yeye na mume wake wakamfuata kumuuliza lakini alikakataa na kumazimu kwenda kwa mjumbe.
Amesema ana wasiwasi kwa kuwa maisha ya sasa yamebadilika si kama zamani na itabidi wakishindwa kuafikiana waende Polisi.
Mama aliyemchukua mtoto kumnyonyesha amesema ameshangazwa na tuhuma hizo kwa kuwa si kweli kwani yeye alishaacha kumnyonyesha mtoto wake miezi sita iliyopita, ana akili timamu hawezi kufanya vitu kama hicho..anasema alimchukua na kumpa chakula baada ya kumuona analia na si kumnyonyesha.
Sikiliza tukio zima likizungumziwa hapa…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE