HekaHeka ya leo inamuhusu kaka mmoja ambaye anasimulia kuhusu kumfumania mke wake wa ndoa na mwanaume mwingine ambaye ana asili ya Kihindi.
Anasema pamoja na kushuhudia kuwa mke wake ana uhusiano na mtu mwingine alimsihi kurudi nyumbani kwani bado anampenda lakini mwanamke hakujali na kuendelea kuwa na mwanaume huyo huku akiacha familia yake bila kuijali.
Anasema alianza kuona hizo dalili tangu mwaka jana baada ya kuona mke wake amebadilika na alipofatilia aligundua ni kweli. na ikafika wakati wakagombana na mke wake sana lakini akaamua kuondoka na kwenda kuishi na huyo mwanaume kama mume na mke.
Anasema tayari alishashtaki hadi ustawi wa jamii na yule muhindi aliahidi hatamsumbua tena mke wake lakini anashangaa mpaka sasabado anaendelea.
Isikilize mwenyewe hapa kwenye HekaHeka ya leo.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos