Hekaheka ya leo inatokea Dar es salaam eneo la Tabata Kinyerezi, inamhusu mume kujeruhiwa vibaya sehemu zake za siri na mke wake kisa ni mlevi kupita kiasi.
Mke wake amekua anakerwa na tabia ya mume wake ya ulevi tangu siku nyingi na mara nyingi amekua akimkataza tabia ya kunywa pombe bila mafanikio yoyote.
Mmoja wa ndugu wa karibu amesema siku ya tukio ndugu yake kama kawaida alirudi nyumbani usiku saa mida ya 7 na kumkuta mke wake amelala..kutokana na mkewe kukerwa na harufu ya pombe ya mumewe wakati akimsumbua kutaka kukutana nae kimwili kwa hasira mwanamke huyo akamng’ata sehemu zake za siri na kuanza kutokwa damu nyingi.
Baada ya tukio hilo jamaa huyo alipatwa na maamuzi makali na kuamua kukimbilia hospitali ya Muhimbili ambapo alitibiwa na kuambiwa kutokana na kuvuja damu nyingi hataweza kupata watoto kutokana na hali yake.
Isikilize hapa mtu wangu….
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos