Wiki nzima timu ya Hekaheka ilikua ikizungumzia tukio la mtoto aliyezaliwa kisha mama yake kumwachia daktari na kushindwa kuafikiana hadi mtoto alipotimiza miezi tisa akiwa analelewa chini ya dokta.
Mtoto huyo anatarajiwa kukabidhiwa kwa mama yake leo baada ya kukamilisha taratibu zote … lakini timu ya Hekaheka ikaona izungumze na Maofisa wa ustawi wa jamii ambao wamezungumza mambo mengi ikiwemo taratibu za kuweza kufanywa kabla ya mtoto huyo kukabidhiwa kwa mama yake leo.
Maofisa hao pia wamezungumza taratibu mbalimbali za kuweza kumpea mtoto ambaye ameshindwa kulelewa na wazazi wake, na pia wanafanya kazi na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi katika kuweza kuwahifadhi watoto hao.
Pia wamesema watu kutoka nje wanaweza kupewa watoto waweze kuwalea endapo watakamilisha taratibu zote zinazohitajika ikiwa kupata kibali kutoka Polisi.
Wasikilize hapa wakizungumza kwenye Hekaheka…
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos