Siku ya Alhamis iliyopita kulitokea ajali mbaya ya moto maeneo ya Buguruni na kuteketeza familia ya watu tisa.
Timu ya Hekaheka ilitembea nyumba iliyotekea kwa moto na kukuta majirani wakiwa bado na simanzi kutokana na tukio hilo.
Mjumbe wa eneo lile amezungumza na kusema alishuhudia tukio zima na kusema alikuwa wa kwanza kupiga kelele baada ya kuona moto mkubwa huku akisikia kelele tunakufaaaa…lakini alipotaka kufungua geti tayari ilikua limepata moto sana.
Anasema pamoja na watoto wawili waliokuwa ndani kurusha ufunguo ili wasaidiwe lakini haikuwezekana kutokana na moto kuwazidia na pia kuwepo na shoti na baadaye walisikia mlio mkubwa wa gesi iliyolipuka kisha hawakusikia sauti tena.
Anasema kinachowasikitisha zaidi ni watu wakipita eneo hilo na kuanza kuwatukana kwamba ni kwanini wameshindwa wakati lilikuwa dogo bila kujua lilikuwa limeshika moto na kinapiga shoti.
Wasikilize mashuhuda wa tukio wakizungumza na Geah Habib kwenye HekaHeka…
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michzo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos