Hekaheka ya Jana ilisikika kutoka Mbeya ambapo dada mmoja alishambuliwa kwa chupa na wifi yake hadi kulazwa hospitali kwa madai anamtafutia mdogo wake ambaye ni mume wa wifi yake wanawake.
Leo dada aliyepigwa amezungumza na Hehaheka kuhusu tukio zima lilivyotokea… amedai hakuwahi kuwa na ugomvi wowote na wifi yake huyo ambaye ni mke wa mdogo wake bali alikua akimhisi tu kuwa anatembea naye kitu ambacho si kweli.
Ameeleza kuwa siku ya tukio alikuja gafla kwenye eneo la biashara yake na kuanza kumshambulia kwa chupa kabla ya watu kumwokoa huku hali yake ikiwa mbaya na kulazimika kulazwa hospitali akitibiwa majeraha yake.
Mama mkwe ambaye alipigwa hadi kuzimia naye aliseme alishuhudia mkwe wake akimpiga sana mwanaye kwa kutumia chupa na anashangaa mwanaye ambaye ni mume wa mwanamke aliyempiga mtoto wake kutoonyesha kuumizwa na tukio la dada yake kuumizwa na alikwenda mara moja hospitali kumwona.
Msikilize dada aliyeumizwa akizungumza kwa taabu kutoka hospitali ya Rufaa Mbeya..
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.