Leo ni mwendeleo wa Hekaheka ya jana ya binti aliyekwenda Oman kufanya kazi za ndani lakini kutokana na kutolipwa hela zake aliamua kurudi nyumbani kwao Tanzania.
Alisema alipokuwa huko licha ya kuhaidiwa kutunzwa vizuri alijikuta akiteswa na kupigwa sana makofi baada ya kudai pesa zake na amerudi nyumbani akiwa haongei kabisa wala kusikia.
Mwanamke ambaye alimsafirisha binti huyo alisema Sada alianza kuwa na kiburi na hakuwahi kufanyiwa kitu chochote lakini nao wanashangaa kuona hasikii wala kuongea.
Baada ya kufanyiwa uchunguzi wataalamu wa afya wamesema si rahisi tena msichana huyo kuweza kusikia kutokana na alivyokuwa akifanyiwa.
Wasikilize hapa wakizungumza na Geah Habib
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos