Hekaheka imekua ikituletea matukio mbalimbali yanayotokea katika jamii zetu..Hekaheka ya leo inatokea Maramba Mawili Mbezi,Dar es salaam kuna mtoto wa miaka mitatu amepigwa sana na sasa amelazwa ICU, Muhimbili.
Mama yake alisema baada ya kutoka kucheza na wenzake alirudi nyumbani akiwa hana ndala na mama yake akamtaka arudi kuzichukua lakini hakurudi tena nyumbani na wakaanza kumtafuta bila mafanikio.
Baba yake amezungumza na kusema walimtafuta sana bila mafanikio hadi usiku wa saa 5 na kushauriana waende kutoa taarifa kituo cha Polisi, asubuhi waliendelea kumtafuta mtoto sana lakini ilipofikia jioni wakati wapo kituo cha Polisi walipigiwa simu mtoto kapatikana akiwa na majeraha makubwa.
Wanasema walimkuta kwenye nyumba ambayo haijakamilika akiwa katika hali mbaya sana huku anatokwa damu puani,mdomoni na masikioni huku akiwa amewekewa matofali kwa juu.
Madaktari wamesema ubongo wa mtoto umehama na itachukua siku 21 kuweza kupata fahamu.
Msikilize baba yake mzazi akisimulia tukio hilo…
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos