March 14 2016 kupitia Hekaheka ya Clouds FM, Geah Habib ametuletea Hekaheka iliyotokea Tanga hii ni baada ya ndugu kuchanganya Maiti katika Hospitali ya Bombo, Tanga, wakwanza kuchukua mwili wa marehemu walishamfanyia taratibu za mazishi na kuzika, ndipo badae walipo lazimika kufukua mwili baada ya kugundua siyo ndugu yao.
‘Maeneo ya Mikanjuni kulitoke msiba wa mzee aliyefahamika kwa jina la mzee Mhina ndipo walipompeleka kumuifadhi katika Hospitali ya Bombo, na kesho yake saa nne tulienda kuchukua maiti yetu kwa ajili ya kwenda kuzika tulifanikiwa kuzika lakini badae uongozi wa Bombo ulifika na kutuambia ile maiti sio yetu‘>>> Mkazi
‘Aliyeenda kuchukua mwili wa marehemu Hospitali ni Baba Mdogo, kuuosha pia alisismamia yeye baba mdogo na walivyorudi nyumbani baba mdogo alikata watoto wasione maiti ya baba yao mwisho wa siku ili bidi tufukue tuwape mwili wao na sisi tuchukue mwili wetu‘>>>Shuhuda
Unaweza kusikiliza hapa Full Stori….
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE