Zaidi ya hekta laki nne za misitu hupotea kila mwaka kanda ya mashariki mikoa ya (Morogoro,Pwani na Daresalam) kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo uanzishwaji wa mashamba mapya ya kilimo, ukataji miti kiholela kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa na upasuaji mbao.
Akizungumza kwa niaba ya meneja kanda ya mashariki TFS afisa uhifadhi mkuu Patricia Manonga, ameeleza hali ya misitu kwasasa ambapo amesema hali ya uharibifu wa misitu imekua ikiongezeka kila siku kutokana na wananchi kuendelea kutumia nishati za kuni na mkaa.
Tanzania ina hekta za misitu milioni 48.1 na inachukua asilimia 55 ya ardhi ya taifa hili, ambapo licha ya jitihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na serikali kwa kushirikiana na wakala wa huduma za misitu tanzania na wadau wengine wa mazingira, bado kumendelea kuripotiwa uharibifu wa misitu hapa nchini.
Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima amesema kama Mkoa umejipanga kuhakikisha unadhibiti changamoto hiyo na kurejesha uoto wa Asili ambao umepotea kwenye misitu mingi ya Mkoa huo.
Anasema miaka 40 iliyopita milima ya Uluguru ilikuwa inatiririsha maji nyakati zote lakini hivi sasa hali imekua tofauti hivyo mpango ni kweli kuendelea kupambana na changamoto hiyo.
Katika kuinusuru Tanzania na kiwango hicho kilichokithiri cha uharibifu wa misitu, elimu imeendelea kutolewa kwa jamii kutumia Nishati ya Gesi ikiwa ni moja ya mikakati yakudhibiti uharibifu wa mazingira, matokeo yake kwa baadhi ya taasisi za Elimu yameanza kuonekana ambapo Kaimu Mkurugenzi Kampuni ya Taifa gesi Angel Bhoke anafika Mkoani Morogoro na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali wakiwemo mama lishe pamoja na taasisi zinazohudumia watu wengi wakiwemo shule za bweni,Magereza.
Katika kutoa hamasa wananchi kutumia nishati ya gesi kampuni hiyo imetoa mitungi midogo ya kilo 3 kwa watu zaidi ya mia tatu huku akisitiza kua nishati hiyo ni nzuri na yenye gharama nafuu.
Amina Ally Mmoja wa wananchi waliopata msaada huo wameishukuru kampuni hiyo na kwamba watakua mabalozi kwa wananchi ili kuacha kuharibu misitu kw. Manufaa ya kizazi kijacho.