Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, amesema ni dhamira ya hospitali hiyo, kuwapokea wagonjwa, watakaofikishwa kwa njia ya helikopta.
Amesema hayo, baada ya kukamilisha mazungumzo na wataalam wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), jijini Dar es Salaam.
“MNH-Mloganzila, inaona mazingira yanaweza kukidhi, na tumefanya maamuzi kwa kutengeneza eneo maalumu la kushukia helikopta,” amesema Prof. Janabi