Kiungo wa kati wa Uingereza Jordan Henderson alikamilisha uhamisho wa kwenda kwa wababe wa Uholanzi Ajax Alhamisi jioni, miezi sita tu baada ya kusajiliwa na Al Ettifaq ya Saudi Arabia.
Henderson ametia saini mkataba wa miaka 2 na nusu na klabu ya Eredivisie.
Al Ettifaq walifikia makubaliano ya pande zote kusitisha mkataba wa Henderson mara moja. Henderson, 33, atachukua punguzo kubwa la mshahara kutoka kwa mshahara wake Saudi — unaofikiriwa kuwa angalau pauni 350,000 kwa wiki ($443,000).
“Ningependa kushukuru klabu, mashabiki na wote waliohusika kwa nafasi hii na kuwatakia kila la kheri kwa kipindi kilichosalia cha msimu,” Henderson alisema.
“Kazi kubwa inaendelea ambayo najua italipa siku zijazo.”
Henderson alihamia Saudi Julai mwaka jana kwa mkataba wa miaka mitatu, na kuhitimisha miaka 12 ya kukaa Liverpool, na kuungana tena na meneja wa Al Ettifaq na mchezaji mwenzake wa zamani wa Anfield Steven Gerrard.